Saturday, January 30, 2010

Swali ya Kwanza

Ungeweza kunishi katika enzi/mwaka yoyote, ungechagua gani na kwa nini?

5 comments:

  1. http://www.stanford.edu/~mbourbon/enzi%20ya%20kuishi.m4a

    ReplyDelete
  2. Uki"cutandpaste" URL hii, utaweza kusikiliza jibu yangu. :)

    ReplyDelete
  3. Kama ningeweza kuchagua kuishi katika enzi yoyote, nasema kwamba ningependa kuisha katika mwaka huu, sasa hivi! Najua kama swali yako ni kufikiri kuhusu enzi yoyote na historia, lakini nasema pia kwamba sasa hivi ni muda mzuri kabisa! Kuna vitu vingi duniani ambavyo vinabadilisha sana kwa sasa - mabadiliko ya hali ya hewa, siasa, sayansi - kila kitu ni kubadilisha na kila kitu ni kusisimua. sasa kuna fursa nyingi za kushiriki katika njia ya dunia itakuwa. hasa kwa sababu kuna fursa nyingi za kushiriki katika njia ya dunia itakuwa. - Deshka

    ReplyDelete
  4. Kipindi ambacho ningependa kuishi.
    Kama ningependa kuishi, ningependa kuishi katika kipindi cha zama za mawe. Ningependa kuishi katika kipindi hiki kwa kuwa, ktika kipindi hiki, kila kitu kilitengeneza kwa kutumia mawe. Hakukuwepo na haja ya kuwa na teknolojia kubwa sana kama ilivyo sasa hivi.
    Katika kipini hicho, watu waliishi kuwa kula matunda na mizizi. Hakukuwepo na vyakula vinavyotengenezwa viwandani; vyakula ambavyo vinaweza kumsababishia binadamu madhara katika mwili.
    Katika kipindi hicho, watu waliishi kwa kuwinda wanyama wa porini bure. Mtu hakuhitaji kuwa na leseni kuwinda wanyama. Na katika kipindi hicho, watu walikuwa wakila nyama bure.
    Kipindi hicho kilikuwa kizuri kwa kuwa watu walikuwa hawawazi sana kuhusu matumizi ya pesa. Enzi hizo, pesa zinazotumika sasa hivi, zilikuwa bado hazijavumbuliwa. Watu waliishi kwa kubadilishana malighafi. Kwa mfano, mtu akiwa na nyama, anabadilishana na mtu mwenye chakula na maisha yanaendelea.
    Katika kipindi hicho, hakukuwepo na mawazo ya elimu rasmi. Siku hizi, watu wanasema bila elimu rasmi huwezi kuishi maisha mazuri. Enzi za zama za mawe, watu walikuwa wakiishi kwa elimu isiyo rasmi.Watoto walikuwa wakizifunza kwa kuwaangalia wakubwa wao ama kutokana na hadithi walizokuwa wanahadithiwa na mababu zao.
    Wakati wa enzi za mawe, kulikuwa hakuna uchafuzi wa mazingira wala mambo ya globalizesheni. Watu walikuwa hawana magari, ndege, na pia hakukuwepo na viwanda kama sasa. Viwanda na moshi wa magari vinachafua mazingira na kuyafanya kmaisha ya binadamu kuwa hatarini.
    Wakati wa zama za mawe, watu walikuwa wakiishi kama familia ama jumuiya moja; wakisaidiana katika shida na raha. Wakati huu, watu wanaishi kila mmoja peke yake na kama una matatizo ama ugonjwa, unaweza ukajifia bila jirani yako kujali kama unaumwa.

    Wakati wa enzi za mawe, watu hawakujali sana kuhusu mahali pa kuishi. Mtu angeweza kuishi kwenye mti; mwingine akaishi pangoni na mwingine akaishi popote pale alipokuwa anaona panamfaa. Siku watu wengi wanapenda kuishi maeneo ya mijini; sehemu ambazo kila aina ya huduma inapatikana.

    Siku njema.

    ReplyDelete
  5. Ningependa kuishii wakati wa enzi ya Malkia Elizabeth wa Kwanza. Ningependa kuishii wakati wa utawala wake kwa sababu ningependa kukutana na Shakespeare. Shakespeare alikuwa mwandishi anayeandika vitabu vyingi kama “Romeo na Juliet.” Napenda pia nguo za enzi hii. Nafikiri utamaduni wa utawala wa Elizabeth ulikuwa mzuri sana. Ningependa pia kuona vita baina ya Uhispania na Uiingereza.

    Ikiwa nisingeishii wakati wa enzi ya Malkia Elizabeth ningependa kuishi miaka sitini katika Marekani. Ningelalamika dhidi ya vita vya Vietnam. Ningekutana na “Hippies.” Ningepiga kora kwa JFK. Ningesikia na musiki ya “Folk.”

    Swahili mzuri!

    Keren

    ReplyDelete